Cipriano Cassama, ajiuzulu Urais baada ya siku moja tu kupita tangu kukaa madarakani


Cipriano Cassama ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Urais, Guinea-Bissau baada ya kukaa madarakani kwa siku moja, akisema maisha yake yalikuwa hatarini.

Image result for Cipriano Cassamá

Cipriano Cassama alichaguliwa na wabunge kuwa rais wa mpito baada ya chaguzi zilizo susiwa mwezi Disemba.

”Leo hii maisha yangu yamekuwa hatarini, familia yangu imekuwa hatarini, maisha ya watu wengi yamekuwa hatarini pia, na ndiyo maana nimeamua kujiuzulu.” amesema

Hatua hii ni pamoja na ukweli kuwa Jenerali wa jeshi wa zamani Umaro Cissoko Embaló tayari alikwisha apishwa kuwa rais katika hoteli mji mkuu wa nchi hiyo, Bissau.

Kwa mujibu wa BBC, Guinea-Bissau imekutwa na matukio tisa ya mapinduzi tangu mwaka 1980. Koloni hilo la zamani la Ureno, pia limekuwa njia ya usafirishaji wa madawa ya kulevya kutoka Amerika Kusini yakielekea Ulaya.

Kwanini Guinea-Bissau ina marais wawili?

Kura zilikusudiwa kufuta kumbukumbu ya yaliyopita, lakini badala yake, zimesababisha mgogoro mpya wa kisiasa katika taifa ambalo Jeshi limekuwa na ushawishi wa kisiasa.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza bwana Embalo kuwa amemshinda mpinzani wake, Domingos Simoes Pereira kwa asilimia 54% kwa 46% katika uchaguzi wa duru ya pili mwezi Disemba tarehe 29.Wafuasi wa bwana Embaló wakishangilia baada ya kutangazwa mshindiWafuasi wa bwana Embaló wakishangilia baada ya kutangazwa mshindi

Rais aliyeondoka madarakani José Mário Vaz alikabidhi madaraka kwa Bwana Embaló katika sherehe zilizofanyika katika hoteli ya kifahari siku ya Alhamisi.

Lakini Bwana Pereira wa chama cha PAIGC, kilichoiongoza Guinea-Bissau kupata uhuru wake na kilichokuwa pekee mpaka 1990, alikataa kuapishwa kwa Embaló, akisema uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.

Kisha kikatumia wingi wa idadi ya wabunge kumuapisha bwana Cassamá, spika wa bunge kuwa rais wa mpito, mpaka Mahakama ya juu ilipotoa uamuzi kuhusu ombi la kubatilisha ushindi wa Embaló.

Cassamá amesema nini?

Bwana Cassamá amesema hakuwa na cha kufanya isipokuwa kuondoka madarakani kwa kuwa amekuwa akikabiliwa na vitisho vya kuuawa.

”Sina ulinzi. Maisha yangu yako hatarini, maisha ya familia yangu yako hatarini,maisha ya watu wa taifa hili yako hatarini. Siwezi kukubali hali hii, ndio sababu nikachukua uamuzi huu,” aliwaambia waandishi wa habari.

Cassamá hakusema ni nani aliyemtishia maisha yake. Mmoja wao, Aristides Gomes, alisema maafisa wa jeshi walivamia nyumbani kwake mjini Bissau ili kumshurutisha ajiuzulu.

”Walitishia kuwaua maafisa wa usalama ikiwa hawatajiuzulu, na kunitishia kuniua kama sitajiuzulu nafasi ambayo nilipatiwa kwa muibu wa sheria,” alisema.

Jumuia ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika (Ecowas), imetoa wito wa kusitishwa mvutano huo.

Bwana Embaló amesema anataka kutatua mzozo na kuipatia maendeleo Guinea-Bissau, moja kati ya nchi masikini duniani, iliyo na watu ilioni 1.6.